Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi
Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Umoja wa Wakerekewa na wana maskani wa
CCM wa Umoja wa Askari wastaafu Kijangwani hapo nyumbani kwake katika hafla ya
kuwakabidhi msaada kwa ajili yakuimarisha Umoja wao.
Picha na
Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali
Iddi amewahimiza wanachama wa Vikundi,
Jumuiya na Taasisi za Chama hicho kuendelea kukilinda na kukitetea chama chao
muda wote ili kiwe na uhakika wa kuongoza Taifa hili Bara na Zanzibar.
Alisema kazi
zinazofanywa na taasisi pamoja na jumuiya hiyo zinaeleweka vyema ndani ya Uongozi
wa Chama ngazi zote jambo ambalo viongozi hao wanawajibika kuzisaidia kwa hali
yo yote ile.
Balozi Seif
ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar aliitoa kauli hiyo wakati
akikabidhi msaada wa Viti 50, Mabusati 20 na mipira sita kwa Umoja wa
wakereketwa na wanamaskani waliochini ya Umoja wa Maaskari wastaafu uliopo Kijangwani
Mjini Zanzibar.
Msaada huo
ulienda sambamba na Balozi Seif kukabidhi jumla ya shilingi laki tano taslimu
kwa Vijana Msimamo Saccos iliyomo ndani ya Umoja huo vyote vikiwa na thamani ya
shilingi Milioni 1,380,000/-.
Aliwapongeza
wanachama wa umoja huo kwa uwamuzi wao wa kuazisha taasisi hizo zikiwa na lengo
la kuongeza mitaji itakayosaidia wanachama hao kupunguza ukali wa maisha
sambamba na kulinda uhai wa Chama chao.
Alieleza
kwamba suala la kuanzishwa saccos miongoni mwa wanachama wa vyama vya siasa na
hata wananchi katika maeneo mbali mbali nchini limo ndani ya ilani ya CCM na kuendelea
kusisitizwa kila mara na Serikali zote
mbili.
“ Kazi
mnazozifanya katika jumuia zenu zikiwemo zile za uzalishaji zilizobebwa ndani
ya vikundi vya saccos zinaeleweka na kuthaminiwa na Serikali na ndio maana ukaanzishwa mfuko maalum wa
J.K na A.K “. Alisisitiza Mjumbe huyo wa
Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif.
Balozi Seif
alisisitiza kwamba Serikali wakati wote zinaendelea kuunga mkono juhudi za
Wananchi walioamua kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali kwa lengo la
kujisaidia kimapato.
“ Popote
pale mnapooona mnakwama katika kuendeleza shughuli zenu za kila siku
tafadhalini msisite kuniona au kuniandikia tutafute namna au mbinu za kuzitatuz
changamoto zenu “ Alifafanua Balozi Seif.
Akipokea
msaada huo Mjumbe wa Kamati ya Umoja Wakerekewa na wana maskani wa CCM wa Umoja
wa Askari wastaafu Ndugu Ali Ahmada
alimshukuru Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi
Seif kwa jitihada zake za kusaidia jumuia za Chama hicho.
Nd. Ahmada
alisema hatua hiyo ya Balozi Seif mbali ya kuleta faraja kwa wanachama wa
jumuiya hizo lakini pia inasaidia kuimarisha nguvu za Chama cha Mapinduzi
katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Mapema
Mshika fedha wa Vijana Msimamo Saccoc Nd. Ramadhan Saleh Abdulla { Barongo } alisema saccoc yao
imeundwa ili kuwakusanya vijana wapate muda wa kufanya shughuli mbali mbali
zitakazosaidia kuwapatia vipato na kuondokana na tabia ya kuzurura mitaani.
Nd. Ramadhan
alisema vijana hao wamefikia auamuzi huo baada ya kuelewa kwamba hawatakuwa na
uwezo wa kupata ajira kutoka serikalini.
Othman
Khamis Ame
Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
8/12/2013.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni