Uwanja wa FNB utakaofanyika Ibada ya Kitaifa ya Kumbukumbu ya Mandela
Maelfu ya waombolezaji wanatarajiwa
kuwepo Jijiji Johannesburg kuhudhuria Ibada ya kitaifa ya kumbukumbu
ya Nelson Mandela itakayofanyika leo.
Rais wa Marekani Barack Obama pamoja na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon watakuwa miongoni mwa
waombolezaji.
Ibada hiyo itafanyika kwenye uwanja wa
FNB, wenye uwezo wa kuingiza watu 90,000 ambao ndio ambao Mandela
alitoa hotuba yake ya kwanza kwa umma.
Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini
alifariki dunia Desemba 5, akiwa na umri wa miaka 95 na anatarajiwa
kuzikwa Desemba 15.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni