Washindi wa Mbio ndefu za KM 42 katika
Mashindano ya Uhuru Marathon wakiwa wamesimama mbele ya mgeni
rasmi, mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Mshindi wa Kwanza ni Jamin
Ikai (kutoka Kenya), Steven Selevestor (kutoka Jeshi la Magereza
Tanzania) pamoja na Aley Sanka (Tanzania).
Washindi wa Mbio ndefu za KM 42
(wanawake) wakiwa wakiwa wamesimama mbele ya mgeni rasmi, mara baada
ya kukabidhiwa zawadi zao.Mshindi wa Kwanza ni Thabita Kibet
(kutoka Kenya), Naum Jerkosgei (Kenya) pamoja na Banoela Brigton.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Mbio
za Uhuru Marathon,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa hotuba yake wakati wa
maadhimisho mbio hizo zilizofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders
Club, Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania.
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dkt. Fenella Mukangara akisoma hotuba yake kabla ya
kumkaribisha Mgeni Rasmi, wakati wa maadhimisho mbio hizo
zilizofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Jijini
Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa
Tanzania.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni