Zlatan Ibrahimovic alipachika wavuni
mabao mawili mnamo dakika za mwisho na kutengeneza mengine mawili
wakati Paris St Germain ikiiadhibu Sochaux kwa ushindi wa mabao 5-0,
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1.
Ibrahimovic alipachika mabao mawili
katika dakika za mwisho za 87 na kuelekea kumalizika kwa mchezo huo,
huku akiwa tayari alishawatengenezea mabao Thiago Silva na Edinson
Cavani katika mchezo ambao Ezequiel Lavezzi nae alifunga bao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni