Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
wamemchagua Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu Mwenyekiti wa bunge hilo.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa
Uchaguzi alisema Samia Suluhu Hassan amepata kura 390 sawa na
asilimia 74.6, Amina Hassan Amour kura kura 126 sawa na asilimia
24.1, kura zilizoharibika zilikuwa kura 7 na jumla ya wajumbe 523
walipiga kura.
Sasa Bunge hilo limepata Mwenyekiti
wake Samwel Sitta aliyechaguliwa jana kuwa Mwenyekiti ambaye
anaungana na Samia Suluhu Hassan aliyechaguliwa leo kuwa Makamu
Mwenyekiti.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni