Andy Murray ameepuka kutumbukia katika
orodha ya majina makubwa yalioanza vibaya baada kuibuka na ushindi wa
seti nne dhidi ya Andrey Golubev wa Kazakhstan katika michuano ya
Wazi ya Ufaransa.
Muingereza Murray alishinda kwa seti
6-1 6-4 3-6 6-3 dhidi ya Golubev ambaye ni mchezaji namba 53 katika
viwango vya dunia katika uwanja Suzanne Lenglen.
Ushindi huo wa Murray ni wa kwanza
katika Roland Garros tangu mwaka 2012, baada ya kukosa michuano hiyo
kutokana na maumivu ya mgongo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni