Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Ujerumani
itakayo cheza michuano ya kombe la dunia Julian Draxler na Benedikt
Howedes, wamepata ajali pamoja na dereva wa mbio za magari za langa
langa Nico Rosberg wakati wakipiga picha ya promosheni ya Mercedes.
Rosberg na dereva wa DTM Pascal
Wehrlein walikuwa wamewapakia wachezaji hao wa Ujerumani Draxler na
Howedes kwenye magari tofauti wakati gari la Wehrlein lilipogonga
watu wawili barabarani Kusini mwa Italia, mkoa wa Tyrol.
Rosberg, Wehrlein, Draxler pamoja
Howedes hawakujeruhiwa katika ajali hiyo ambayo haikutarajiwa
kutokana na barabara hiyo kuwa ilikuwa imefungwa kwa matumizi ili
kufanya tangazo hilo la Mercedes.
Benedikt Howedes Julian Draxler
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni