Luis Suarez ametuma ujumbe kwa
wachezaji wenzake wa Liverpool walio kwenye kikosi cha Uingereza na
kutahadharisha kuwa atakuwa yupo fiti wakati Uingereza itakapochuana
na Uruguay katika michuano ya Kombe la Dunia.
Mchezaji huyo bora wa mwaka wa Ligi Kuu
ya Uingereza, alifanyiwa upasuaji wa kwenye goti baada ya kuumia
katika mazoezi, amewatumia ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu
rafiki zake wa Anfield kuwa watakutana Juni 19, huko Sao Paulo.
Daktari wa timu ya Uruguay, Alberto
Pan amethibitisha jana kuwa Suarez anaendelea vizuri, baada ya
kufanyiwa upasuaji huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni