Nchi ya China imekanusha mashtaka
yaliyofunguliwa na Marekani dhidi ya maafisa wake wa jeshi kuhusika
na wizi wa kimtandao wa nyaraka za biashara za makampuni matano.
Serikali ya China imesema haijawahi
kujihusisha wala kushiriki katika wizi wa kimtandao, na kuongeza kuwa
mashtaka hayo ya Marekani yataharibu uhusiano wao.
Aidha, China imemuita balozi wa
Marekani kufika Beijing kutoa maelezo kuhusiana na kitendo hicho cha
nchi yake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni