Mkuu wa Jeshi la Thailand amepiga
marufuku vyombo vya habari kuripoti jambo lolote linaloweza
kuhatarisha usalama wa taifa la nchi hiyo, hatua inayokuja baada ya
jeshi kuamua kutwaa madaraka ya nchi hiyo.
Umamuzi huo kushtukiza wa jeshi
kutwaa madaraka, unalipa jeshi la Thailand madaraka makubwa ya
kutekelezwa kwa maamuzi yake.
Jeshi la Thailand limesisitiza
walichofanya ni kubeba majukumu ya kuleta utulivu ana amani ya nchi
hiyo kutokana na mgogoro wa muda mrefu wa kisiasa na wala si
mapinduzi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni