Mahakama nchini Uganda imemuhukumu
kifungo cha miaka mitatu jela muuguzi kwa uzembe uliopelekea uwezekano wa
kumuambukiza virusi vya Ukimwi mtoto wa kiume wa miaka miwili.
Muuguzi huyo Rosemary Namubiru,
ambaye anaishi na virusi vya Ukimwi, alitumia kumchoma sindano mtoto
huyo ambayo alijichoma yeye kimamkosa kidoleni.
Wanaharakati wameshutumu hukumu
hiyo, kutokana na mtoto huyo kutoambukizwa virusi vya Ukimwi katika
tukio hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni