Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Rahma Ngassa (Kulia), akiwaeleza wanafunzi hawa jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na uanachama wa Mfuko huo, wakati wa maonyesho ya vyuo vya elimu ya juu yaliyoandaliwa na Tume ya vyuo vikuu (TCU), kwa kushirikiana na wizara ya elimu na mafunzo yan ufundi stadi. Maonyesho hayo ya siku tatu yamefunguliwa jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Frederick Mossi (Kushoto) na Afisa Masoko wa Mfuko huo, Rahma Ngassa (Kulia), wakiwaeleza faida mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo kwa wanachama wake, baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya siku tatu ya taasisi za elimu ya juu kwenye ukumb i wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Mfuko wa Pesnheni wa PSPF (Kulia), wakitoa maelezo kwa baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya siku tatu ya taasisi za elimu ya juu na kufanyika kwenye ukumbni wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yaliyofunguliwa jana, yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni