Wadau wa Bandari na Reli wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Taasisi ya Uwekezaji katika nchi zinazoendelea ya Ubelgiji (BIO)baada ya kumaliza kikao cha kuishawishi taasisi hiyo kuwekeza katika miradi mbalimbali ya kukuza uchumi na kupambana na umaskini Tanzania.
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi za bendera ya taifa) ameongoza ujumbe huo. Aidha, Balozi Kamala amemuomba Bwana. Luik Zonneveld Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo (kushoto kwa Balozi Kamala) kushirikiana na Tanzania kutafuta fedha za kuwekeza katika miradi mikubwa ya reli na bandari Tanzania.
Mkurugenzi huyo amekubali ombi la Balozi Kamala
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni