Mh.Saada M.Salum akifafanua jambo katika moja ya Mikutano ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na watendaji wa mashirika mbalimbali ya Kimataifa,Kulia kwa Mh.Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha – Dkt. Servacius Likwelile na Kushoto ni Bwa.Peter Noni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasimali Tanzania (TIB).
Mh.Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Washiriki mbalimbali wa Mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo uliofunguliwa na Mh.Paul Kagame katika ukumbi wa Mount Karisimbi Jijini Kigali Rwanda.
Na Mwandishi wetu, Kigali, Rwanda
Serikali ya Tanzania ipo imara katika kuendelea na kusimamia juhudi zinazofanywa na Banki ya Afrika katika kuinua mitaji kupitia mpango wa sita wa kukuza mitaji wa benki hiyo (GCI-VI).
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alipokuwa akitoa hotuba yake kwa Magavana wa nchi za Afrika katika mkutano wa mwaka wa wadau wa Benki ya Afrika jijini Kigali, Rwanda.
Mh.Saada amesema kuwa kupitia mpango wa GCI-VI Tanzania imekuwa na uwezo wa kulipa hisa zake zipatazo Dola za Kimarekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda uliopangwa.
Saada amesema kuwa kupitia mpango wa GCI-VI Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kulipa hisa zake zipatazo Dola za Kimarekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda uliopangwa.
Zaidi ya hayo, Waziri Saada ameendelea kusema kuwa nchi yake imeweza kulipa hisa zake za awamu ya nne zipatazo kiasi cha Dola za Kimareka 1,279.30 kabala ya muda uliopangwa.
“Ninaamini ni katika mkutano huu tunaweza kujadili dira ya Benki katika miaka mingine 50 ijayo kama kauli mbiu ya mkutano huu inavyothibitisha, “Afrika tunayoitaka miaka 50 ijayo” alisema Waziri Saada.
Aidha, Waziri Saada alimpongeza Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Donald Kaberuka na uongozi mzima kwa kusimamia na kuongoza kwa umahiri mkubwa majukumu walionayo ya kibenki na kuhakikisha inasonga mbele daima na kuifanya kuwa benki bora barani humu.
Ili kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa bara hili lazima kudumisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kijamii na kujipatia maendeleo endelevu kwa nchi zao na watu wake. Mwaka huu Benki ya Afrika inafikisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwake ambapo imeendelea kuhudumia bara hili kwa mafanikio makubwa.
Kwa upande wake Rais wa Rwanda Paul Kagame akifungua mkutano huo alisema kuwa ili kufikia uchumi wa kati katika Bara la Afrika kwa miaka 50 ijayo inabidi nguvu kubwa ielekezwe kwenye sekta binafsi ambayo itatengeneza ajira kwa vijana na wanawake.
Mkutano huo ni wa siku tano kuanzia 19 hadi 23 Mei mwaka huu ambapo kabla ya ufunguzi wa Mkutano huu ulitanguliwa na mikutano mbalimbali ya Magavana ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiambatana na wajumbe kuwakilisha nchi zao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni