.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 24 Mei 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA, ENG. STELLA MANYANYA ALA KIAPO RASMI CHA UHANDISI


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (PE. 1656) akila kiapo rasmi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian Matembele kwa mujibu wa sheria ya usajili wa wahandisi (Engineer’s Registration Act (Cap 63), Kanuni na sheria ndogo zote zilizowekwa na zitakazowekwa ikiwemo mwendo wa utendaji kazi pamoja na maadili katika taaluma ya uhandisi.
Kiapo hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa “video comference” uliopo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo tarehe 23-05-2014. Awali kiapo hicho kilikuwa kifanyike Dodoma pamoja na mawaziri na wabunge wengine ambao ni wahandisi lakini kutokana na majukumu yasiyozuilika Eng. Manyanya ameruhusiwa aape akiwa Sumbawanga. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian Matembele wakisaini hati ya kiapo hicho mbele ya mashuhuda mbalimbali walioalikwa katika hafla hiyo fupi.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa, pamoja na mambo mengine amesema ni marufuku kwa wahandisi ambao hawajasajiliwa kuidhinisha au kupitisha kazi za miradi mikubwa katika Mkoa wake wa Rukwa.

Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanyana baadhi ya wahandisi waliosajiliwa na ambao hawajasajiliwa kutoka Mkoa wa Rukwa (nyuma waliosimama) muda mfupi baada ya kuapishwa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni