Mshambuliaji wa Chelsea Romelu
Lukaku amefunga mabao matatu yaani hat-trick na kuisaidia timu yake
ya Taifa la Ubelgiji kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya
majirani zao Luxembourg.
Katika mchezo huo kinda wa
Manchester United, Adnan Januzaj alicheza mchezo wake wa kwanza wa
kimataifa baada ya kuingia katika mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa
Ubelgiji.
Winga wa Tottenham, Nacer Chadli
pamoja na aliyekuwa kiungo wa Chelsea, Kevin De Bruyne walifunga goli
moja kila moja katika mchezo huo ambao Belgium walipata ushindi huo
wa kishindo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni