Mwanamke mwenye ujauzito wa miezi mtatu
ameuwawa kwa kupigwa na matofari nchini Pakistan na watu wa familia
yake kutokana na kuolewa na mwanaume aliyemchagua mwenyewe.
Mpelelezi Mkuu Rana Akhtar amesema
mwanamke huyo Farzana Bibi, alishambuliwa kwa matofali nje ya
mahakama kuu huko Lahore High, na watu zaidi ya 12 akiwemo baba yake
mzazi na kaka yake.
Farzana alienda mahakamani kumtetea mumewe
mpya dhidi ya madai yaliyotolewa na familia yake kuwa alitekwa na
mwanaume huyo na kumlazimisha amuoe.
Baada ya tukio hilo baba wa marehemu
alijisalimisha, hata hivyo kaka yake na aliyekuwa mchumba wake
walikimbia na bado hawajatiwa nguvuni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni