Matukio ya kigaidi yaliyoiandama nchi ya Kenya kwa siku za karibuni, yamesababisha kupungua kwa watalii kwa kiasi kikubwa nchini humo hasa katika mji wa kitalii wa Mombasa.
Hali hiyo itasababisha zaidi ya wafanyakazi 4,000 wanaofanya kazi katika hotel za kitalii kupoteza ajira zao kufuatia kupungua sana kwa watalii kutoka nchi za Uingereza, Marekani, Ufaransa na Australia mapema mwezi huu.
Kwa siku za karibuni Kenya imekuwa ikishuhudia milipuko ya mabomu katika sehemu mbalimbali hasa katika miji ya Nairobi na Mombasa inayosadikiwa kufanywa na kundi la Al Shaabab.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni