Zaidi ya watu 118 wamefariki dunia baada ya mabomu mawili yaliyokuwa yametegwa katika magari mawili tofauti kulipuka katika stendi ya mabasi na soko katika mji wa Jos nchini Nigeria.
Hata hivyo taarifa zinasema kuwa, vifo vinaweza kuwa zaidi ya 118, kutokana na ukweli kwamba baadhi ya majengo yaliporomoka kufuatia milipuko hiyo, hivyo uhenda baadhi ya watu wamebanwa katika majengo hayo. Mabomu hayo yalipishana muda wa nusu saa tu wakati wa kulipuka kwake.
Inasadikiwa kuwa, kikundi cha Boko Haramu ndicho kilichohusika katika milipuko hiyo iliyotokea jana.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni