Luis Suarez haofii ubutu wake wa
kutofumania nyavu tangu aanze maisha akiwa na Barcelona ambapo
amesisitiza ushirikiano wake na Lionel Messi pamoja na Neymar
utafanyakazi.
Mshambuliaji huyo amecheza michezo
miwili ya La Liga , tangu ahame kutoka Liverpool na Barcelona
wamepoteza mechi zote mbili alizocheza, dhidi ya wapinzani wao Real
Madrid na Celta Vigo.
Akiongea kabla ya mchezo wao na timu
yake ya zamani ya Ajax, wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Suarez, amesema
daima amekuwa akiota kuichezea Barcelona na kuongeza kuwa atakuwa
fiti katika klabu hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni