Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Thailand
Bi. Yingluck Shinawatra, atakabiliwa na makosa ya uhalifu kutokana na
utata uliogubika kutolewa kwa ruzuku kwa mradi wa zao la mchele.
Taarifa hizo zimetolewa wakati
wabunge wakijiandaa kupiga kura ya kumshtaki Bi. Yingluck kwa
kushindwa kutimiza wajibu wake kuhusiana na mradi huo.
Wakosoaji wa mambo wanasema sera ya
mchele iliigharimu serikali mabilioni na ilitumika kuchota fedha kwa
ajili ya chama cha Bi.Yingluck.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni