.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 23 Januari 2015

MSHAURI WA USALAMA WA NIGERIA ASHAURI UCHAGUZI UHAIRISHWE

Mshauri wa Usalama wa Nigeria Bw. Sambo Dasuki ameisihi tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kuchelewesha uchaguzi mkuu ili kutoa fursa ya kusambazwa kwa kadi za wapiga kura.

Uchaguzi huo ni wa kwanza kwa taifa la Nigeria, ambao unahitaji mpiga kura kuwa na kadi ya
biometric.

Nigeria inayokabiliwa na ghasia zinazotokana na machafuko yanayofanywa na kundi la Boko Haram, inatarajia kufanya uchaguzi wake Februari 14.

Mkuu huyo wa Usalama Sambo Dasuki, pia amesema nchi jirani ya Chad, itatuma kikosi chake kusaidia kupambana na wapiganaji wa Boko Haram ambao wanashikilia miji mingi na vijiji.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni