Majambazi sita wamepigwa risasi na
kufa jana usiku baada ya polisi kuzima mipango yao ya wizi katika
eneo Membley, barabara ya Ruiru-Kahawa Jijini Nairobi.
Majambazi hao wote wanaume walikuwa
kwenye gari aina ya saloon, iliyokuwa ikifuatiliwa na polisi ambapo
mmoja wao aliyekuwa na silaha aina ya AK-47 alitoroka baada ya
kulifyatulia risasi gari la polisi.
Afisa wa kitengo cha uhalifu amesema
walipata taarifa kuwa majambazi hao walikuwa wanapanga kuweka kizuizi
barabarani na kuwaibia wenye magari watakaopita barabara hiyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni