.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Januari 2015

BAADA YA KIPIGO VAN GAAL AJITETEA KUTOMCHEZESHA RADAMEL FALCAO

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal, amejitetea kwa kutomchezesha mshambuliaji Radamel Falcao katika kikosi chake kilicholala nyumbani kwa bao 1 dhidi ya Southampton, kuwa kulitokana na sababu za kiufundi.

Falcao, ambaye alianza kucheza katika michezo mitano iliyopita jana alikaa benchi na kuishia kushuhudia Manchester United ikipoteza mechi hiyo ya ligi kuu ya Uingereza.

Mchezaji huyo wa Colombia anayelipwa paundi 265,000 kwa wiki, alijiunga na United kwa mkopo akitokea Monaco, ikiwa ni mwaka mmoja kupita tangu ajiunge na timu hiyo ya Ufaransa kwa uhamisho wa paundi milioni 50.
                     Jose Fonte akimdhibiti Robin van Persie asilete madhara langoni 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni