.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 19 Januari 2015

BOKO HARAM WATEKA WATOTO KATIKA KIJIJI KILICHOPO CAMEROON

Wapiganaji wanaohisiwa ni wafuasi wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria, wameteka makumi ya watu baada ya kufanya uvamizi katika nchi jirani ya Cameroon.

Mamlaka zimesema wengi wa waliotekwa katika uvamizi huo uliofanyika katika kijiji kimoja mpakani, ni watoto.

Vyanzo vya usalama vimesema wanakijiji wanne waliojaribu kujitetea kukabiliana na washambuliaji waliuwawa.

Boko Haram wanamiliki miji na vijiji kaskazini-mashariki mwa Nigeria, na wameanza kuwa tishio kwa nchi jirani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni