.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 18 Januari 2015

BRAZILI NA UHOLANZI ZAKERWA NA KITENDO CHA RAIA WAO KUUWAWA INDONESIA

Brazili na Uholanzi zimewaita mabalozi wao waliopo nchini Indonesia, baada ya kuchukizwa na serikali ya nchi hiyo kupuuzia maombi ya nchi hizo na kutekeleza adhabu ya kifo kwa kupigwa risasi watu sita waliotiwa hatiani kwa dawa za kulevya wakiwemo raia wawili wa nchi hizo.

Waliotiwa hatiani na kuuwa mbali na raia wa Brazili na Uholanzi, pia yupo raia wa Vietnam, Malawi, Nigeria, pamoja na raia mmoja wa Indonesian, ikiwa ni hukumu za kwanza za kifo kutekelezwa chini ya rais mpya Joko Widodo.

Nchi ya Indonesia inasheria kali dhidi ya dawa za kulevya na rais Widodo, aliyeingia madarakani Oktoba mwaka jana amewakera wanaharakati kwa kuonyesha kuunga mkono adhabu ya kifo licha ya kuonekana ni mwanamageuzi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni