Bondia Deontay Wilder ametwaa taji
la ubingwa wa uzito wa juu duniani kwa kumshinda Bermane Stiverne kwa
pointi kadhaa.
Katika mchezo wao uliochezwa Jijini
Las Vegas Wilder alipata pointi 118-109, 119-108 na 120-107 kutoka
kwa marefa wote watatu dhidi ya mpinzani wake Stiverne.
Kwa ushindi huo Deontay Wilder
anakuwa Mmarekani wa kwanza kushinda taji la uzito wa juu duniani
baada ya kupita zaidi ya miaka nane.
Wilder akimpatia konde la kushoto Steverne
Steverne akimkumbatia Wilder na kuanguka nae
Refa na mabondi wote wakiwa chini baada ya kuangukiana




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni