.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 18 Januari 2015

KOCHA WA CONGO ALALAMIKIA TIMU YAKE KUKAA KWENYE FOLENI MUDA MREFU


Kocha wa Congo Claude LeRoy amekasirishwa na kitendo cha timu yake kukaa barabarani kwa muda mrefu katika basi lenye joto wakati wakielekea katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika.

Katika mchezo huo Congo ilitoka sare ya bao 1-1 na wenyeji Equitorial Guinea, baada ya kufanikiwa kusawazisha katika dakika za mwisho.

LeRoy amesema kwa kawaida safari ya kwenda uwanjani ilikuwa ikiwachukua dakika 12, lakini jana iliwachukua dakika 65 wakiwa kwenye foleni katika basi ambalo halina viyoyozi wakati joto likiwa nyuzi joto 40.

Kocha huyo wa Congo amesema kulipaswa kuwepo kwa jitihada za kuondoa msongamano wa magari ili timu ziweze kufika mapema uwanjani na kutoa wito kwa CAF kuchukua hatua kuhusiana na suala hilo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni