Katika mchezo huo wa ufunguzi, wenyeji Equatorial Guinea ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 16 likifungwa na Nsue Lopez. Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Hata hivyo kipindi cha pili Congo walijibu mapigo na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 87 mfungaji akiwa ni Bifouma Koulossa.
Katika mchezo mwingine wa michauano hiyo ya Mataifa ya Afrika, Burkina Faso walikiona cha moto baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Gabon.
Katika mchezo huo, Gabon walijipatia mabo yao kupitia kwa Pierre-Emerick Aubameyang katika dakika ya 19.
Bao la pili la Gabon lilipatikana katika kipindi cha pili mfungaji akiwa ni Malick Evouna aliyefunga bao dakika ya 72.
Kwa matokeo hayo, Gabon ndiyo inayoongoza kundi A kwa kupata pointi 3 baada ya wenyeji Equatoria Guinea na Congo kutoka sare ya kufungana bao 1-1

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni