Cherif Kouachi, mmoja wa waliohusika
katika kundesha mashambulizi ya kigaidi katika jarida la vibonzo vya
dhiahaka la Charlie Hebdo, amezikwa katika kaburi lisilo na alama
chini ya ulinzi mkali.
Maafisa wa nchi hiyo wamesema
Kouachi amezikwa usiku katika mji wa nyumbani kwao wa kitongoji cha
Gennevilliers, Jijini Paris.
Kaka yake ambaye alishirikiana naye
katika mashambulizi hayo yaliyouwa watu 12, Said Kouachi naye
alizikwa usiku Ijumaa katika eneo la siri mashariki mwa mji wa Reims.
Awali meya wa Reims alikataa kutoa
eneo la kuzikia lakini alilazimwishwa kufanya hivyo kisheria.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni