Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani
Papa Francis ameondoka kuelekea Roma baada ya kuvuta umati mkubwa
wakati wa ziara yake ya siku tano nchini Ufilipino.
Makumi ya maelfu ya watu walijipanga
kando ya barabara kushuhudia msafara wa Papa na kumuona kwa mara ya
mwisho wakati akielekea uwanja wa ndege wa Villamor.
Watu milioni sita hawakujali hali ya
hewa wakati walipohudhuria misa ya eneo la wazi katika Jiji la Manila
hapo jana iliyoongozwa na Papa Francis.
Papa Francis ametumia wiki akiwa
Asia, ambapo pia alitembelea Sri Lanka ambayo ni ukanda unaokua wa
Kanisa Katoliki.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni