.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 21 Januari 2015

RAIA WA MALI APATIWA URAIA WA UFARANSA BAADA YA KUWANUSURU WATU KUUWAWA

Raia wa Mali muislam ambaye aliwanusuru wateja kushambuliwa na mtu mwenye silaha mwenye kufuata itikadi kali za kiislam katika duka la bidhaa la Paris Kosher mwezi huu amepatiwa uraia wa Ufaransa.

Lassana Bathily, 24, ambaye ni mfanyakazi wa duka hilo kubwa la bidhaa alikuwa kwenye chumba cha kuhifadhia bidhaa wakati mtu mwenye silaha Amedy Coulibaly alipovamia duka hilo na kuua watu wanne.

Bathily ambaye alifikiri haraka na kuzima vyumba vya friji katika duka hilo na kisha kuwaficha wateja, amekabidhiwa paspoti na medali ya ushuja na Waziri Mwandamizi wa Ufaransa.

Shambulio hilo la Jijini Paris limeuwa watu 17, huku idadi kubwa walikuwa katika ofisi ya jarida la vibozo la Charlie Hebdo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni