.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Januari 2015

RAIS FRANCOIS HOLLANDE KUONGOZA MKUTANO WA MGOGORO NCHINI UFARANSA HII LEO

Rais Francois Hollande anararajia kuwa mwenyekiti wa mkutano wa mgogoro pamoja na mawaziri wa nchi hiyo kuhusiana na usalama wa taifa hilo baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi wiki iliyopita Jijini Paris.

Mkutano huo umeitishwa huku kikiwa na maswali juu ya ni vipi wapiganaji hao wanaharakati wa Kiislam waliofahamika na mamlaka za nchi hiyo waliweza kutekeleza uvamizi na mauaji hayo Jijini Paris.

Mashambulio hayo ya kigaidi katika jarida la vibonzo la Charlie Hebdo, shambulio lingine la polisi katika tukio tofauti pamoja na katika duka kubwa la bidhaa la kosher yalisababisha vifo vya watu 17. Zaidi ya watu milioni 1.5 waliandamana Jijini Paris jana kuonyesha mshikamano.
         Umati wa watu Jijini Paris katika maandamano ya kuonyesha mshikamano
     Rais Hollande akimkumbatia mwandishi wa jarida la Charlie Hebdo, Patrick Pelloux

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni