Nchi ya Ufaransa kutengeneza ajira
mpya 2,680 na kuongeza matumizi yake kufikia paundi milioni 335 ili
kuboresha mapambano dhidi ya ugaidi, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Manuel
Valls amesema.
Amesema nguvu kazi hiyo ni muhimu
kutokana na kusambaa kwa watu wenye misimamo mikali, ambapo watu
3,000 nchini humo kwa sasa wanapata huduma za kamera za usalama
nchini Ufaransa.
Waziri Mkuu Valls ameeleza hayo
wakati akifafanua mipango ya serikali ya Ufaransa kufuatia tukio la
shambulio la Jijini Paris lililouwa watu 17.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni