.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 22 Januari 2015

UN YASHUTUMU MJUMBE WAO KUITWA KAHABA NA KIONGOZI WA BUDDHA

Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mtaifa ametoa wito kwa Myanmar kushutumu kitendo cha Kiongozi wa Kitaifa wa dhehebu la Buddha wa taifa hilo kumuita mjumbe Maalum wa UN kuwa ni kahaba.

Mkuu huyo wa Haki za Binadamu, Zeid Ra'ad Al Hussein amesema kauli iliyotolewa na kiongozi wa Buddha, Ashin Wirathu inachochea chuki.

Kauli hiyo Wiradhu ilikuwa inamlenga Mjumbe huyo wa Korea Kusini, Bi. Yanghee Lee, ambaye alikuwa ziarani Myanmar wiki iliyopita akijaribu kushughulikia tatizo la kundi dogo la jamii ya Kiislam.

Wirathu aliwahikufungwa jela karibu muongo mmoja kwa kuchochea vurugu za kupinga Uislam.
                                                                          Mjumbe UN Bi. Yanghee Lee

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni