.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 22 Januari 2015

VIDEO INAYOONYESHA POLISI MWEUPE MAREKANI AKIMPIGA RISASI MTU MWEUSI ALIYEJISALIMISHA YATOLEWA

Video imetolewa ikionyesha mwanaume mweusi akipigwa risasi na afisa wa polisi Marekani, wakati akitoka nje ya gari huku mikono yake akiwa amenyoosha juu.

Mwanaume huyo Jerame Reid alikuwa ni abiria katika gari lililoamriwa kusimama na polisi wa Bridgeton, New Jersey, kwa kosa la kukatiza wakati alama ya kusimama ikionyesha.

Kabla ya polisi kumfyatulia risasi mtu huyo afisa mwingine alimtahadharisha mwenzake kuwa ameona silaha kwenye gari hilo.

Tukio hilo linafuatia maandamano ya miezi kadhaa kuhusiana na mauaji wa Marekani weusi wasio na silaha yaliyofanywa na polisi weupe Jijini New York na Ferguson, Missouri.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni