Watu wanne wanaodaiwa kuwa ni
majambazi wameuwawa leo asubuhi kwa kuchomwa moto na wananchi wenye
hasira eneo la Githurai 44, Jijini Nairobi.
Watu hao ambao wote ni wanaume
wanadaiwa kumshambulia na kumpora pikipiki mwendesha bodaboda baada
ya kumchoma kisu na kufa.
Baada ya tukio hilo waendesha
bodaboda waliwasiliana na kuanza kuwatafuta wahalifu hao na
walipowapata waliwashambulia na kisha kuwachoma moto.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni