Wapiga kura nchini Zambia wanapiga kura
katika uchaguzi wa kumchagua rais kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa
nchi hiyo Michael Sata mwaka jana.
Mchuano mkali unatarajiwa kuwa baina ya
mgombea urais Edgar Lungu kutoka chama tawala cha Patriotic Front na
Hakainde Hichilema kutoka chama cha United Party for National
Development.
Mshindi atakayepatikana ataiongoza
Zambia kwa kipindi cha miezi 18 kilichobakia katika muhula wa
marehemu Michael Sata. Wagombea wote wameahidi kuboresha elimu na
kuongeza ajira.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni