Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kurejea dimbani kwa mshambuliaji Daniel Sturridge kumekuwa ndio sababu kuu ya timu hiyo kuimarika kimchezo na kufanya vyema.
Sturridge, alifunga goli jana wakati
Liverpool ikiifunga Crystal Palace mabao 2-1, na kusonga hadi robo
fainali ya kombe la la Chama cha Soka Uingereza FA.
Liverpool imeshinda michezo yake
minne kati ya mitano tangu kurejea dimbani kwa Daniel Sturridge
ambaye alikuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi mitano kutokana na
kuwa majeruhi.
Daniel Sturridge akishangilia goli kwa kucheza staili yake maarufu akiwa na
Alberto Moreno
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni