Vikosi vya jeshi la Nigeria
vimewatimua wapiganaji wa Boko Haram walioshambulia mji wa kaskazini
mashariki wa Gombe.
Wanajeshi na ndege ya kivita
imetumika katika kukabiliana na wapiganaji hao waislam wenye misimamo
mikali katika eneo la kando la mji wa Gombe.
Wapiganaji hao wa Boko Haram
inasemekana wanaonekana kuzidiwa na kusalimu amri katika ngome yao
kuu katika jimbo la Borno.
Nchi ya Nigeria ilihairisha uchaguzi
mkuu uliokuwa ufanywe jumamosi, ili kukabiliaa na wapiganaji wa kundi
hilo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni