Rais wa Ukraine amesema kuwa
makubaliano yakusitisha mapigano na waasi wanaoungwa mkono na Urusi
mashariki mwa nchi hiyo yanapaswa kuheshimiwa na ameagiza jeshi
kuacha mapigano.
Rais Petro Poroshenko pia amewaonya
waasi kuacha kushambulia mji uliozingirwa na mapambano wa Debaltseve.
Mapambano baina ya pande hizo mbili
yameonekana kukoma mara baada ya muda wa kusitisha mapigano
ulipowadia.
Hata hivyo baadae pande zote mbili
za serikali na waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine, walianza
kulaumiana kila mmoja kwa kurusha makombora katika baadhi ya maeneo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni