Polisi Jijini Copenhagen wamesema
wamempiga risasi na kumuua mwanaume mmoja anayeaminika kuwa ndiye
aliyehusika na mashambulizi mawili mabaya katika Mji Mkuu huo wa nchi
ya Denmark saa chache zilizopita.
Polisi wamemuua mwanaume huyo katika
wilaya ya Norrebro, baada ya kuwafyatulia risasi polisi.
Hii ni baada ya kuuwawa kwa mtu
mmoja na kujeruhiwa kwa maafisa polisi watatu, katika mdahalo wa
uhuru wa kuongea katika mgahawa mmoja siku ya jana.
Katika tukio la pili, mwanaume mmoja
Myahudi ameuwawa na polisi wawili kujeruhiwa karibu ya hekalu kuu la
Jijini Copenhagen.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni