Baada ya Rais wa Zimbabwe, Robert
Mugabe kuteleza na kuanguka katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa
Harare, watu wengi duniani wamechukulia kitendo cha kuanguka kwa rais
huyo kama staili ya kutembea wakiwa na lengo la kumdhihaki.
Katika nchi mbalimbali za Afrika na
Ulaya watu wamekuwa wakitembea kama vile wanataka kuanguka
wakimuigiza Rais Mugabe. Rais Mugabe ambaye ameiongoza nchi hiyo
tangu mwaka 1980, alizaliwa Februari 21, 1924, ambapo mwezi huu
atatimiza umri wa miaka 91.
Picha mbalimbali kwenye mitandao ya
kijamii zinaonyesha Mugabe akishiriki shughuli mbalimbali, lakini kwa
stahili kama alivyoanguka uwanja wa ndege.
Kutokana na picha zilizotengenezwa
kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, rais huyo aliagiza
picha hizo zifutwe kwakuwa hazina maana.
Hii ni ya kwenye riadha
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni