Real Madrid imeongeza uongozi wake
wa ligi kuu ya Hispania La Liga kwa tofauti ya pointi nne, baada ya
jana kupata ushindi kupitia mabao ya Isco na Karim Benzema dhidi ya
Deportivo La Coruna katika dimba la Bernabeu.
Hata hivyo katika mchezo huo Real
Madrid haikuonyesha mchezo wa ushindi, kabla ya kurejea kwenye mchezo
wake wa kutetea ubingwa wake wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya
Schalke, katikati ya wiki hii
Katika mchezo huo wachezaji wao
nyota Cristiano Ronaldo na Gareth Bale walikosa magoli baada ya
mashuti yao kugonga nguzom, kabla ya Isco kutumbukiza wavuni goli la
kwanza la Real.
Karim Benzema akiwa wavuni akishangilia goli lake alilofunga
Cristiano Ronaldo akiwa angani akifanya vitu vyake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni