Serikali ya Uganda imejikuta
ikitumia kiasi cha shilingi bilioni 39 za nchi hiyo kila mwaka
kuwatibu vijana wanaotoa mimba kiholela na kupata madhara ya kiafya
kutokana na kufanya ngono zembe.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Straight Talk Foundation Limited, Susan Ajok amesema serikali hutumia
karibu shilingi bilioni 39 kila mwaka kutibu matatizo yatokanayo na
utoaji mimba usio salama ambapo vijana ndio wanaoongoza.
Bi. Ajok ametoa kauli hiyo katika
mkutano wa kuchangisha fedha kusaidia kukabiliana changamoto za
mpango wa uzazi, maisha ya vijana pamoja na mabadiliko ya tabia nchi
uliofanyika Jijini Kampala.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni