Bao la daika ya 36 toka kwa Branislav Ivanovic wa Chelsea ( pichani aliyeruka juu ) liliifanya timu hiyo kuongoza kwa bao 1-0 katika kipindi cha kwanza dhidi ya Paris Saint-Germai ( PSG ) katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo nchini Ufaransa. Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili wenyeji PSG walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 54 kupitia kwa Edinson Cavani huku mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois akiwa hana la kufanya. Hadi mwisho wa mchezo huo timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni