Pichani kulia ni Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, akimkaribisha Mhe. Aboud, Dubai, na kushoto ni Nd. Islam Balhabou
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud, amewasili Dubai kwa ziara ya kikazi.
Akiwa Dubai, Mhe. Aboud atafanya mazungumzo na Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya Dunia 2020 (World Expo2020).
Aidha, atafanya mazungumzo na Nd. Islam Balhabou, Mfanyabiashara Mtanzania ambaye amejitolea kufungua afisi ya biashara ya Zanzibar (Trade Mission).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni