Ujumbe wa NHC ulipokutana na baadhi ya wawekezaji wakubwa wa
sekta ya uendelezaji Miliki wa Singapore ili kuwahamasisha kuwekeza vitega
uchumi vya hoteli nchini Tanzania. Ujumbe huu umekutana na Bw. Henry Ngo ambaye
ni Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bonvest na Hoteli ya Sheraton
Singapore ambao pia wamewekeza Zanzibar Hoteli ya Kitalii.
Ujumbe wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi ukiwa katika Mamlaka ya Uendelezaji wa
nchi ya Singapore(Urban Redevelopment Authority –URA) kujionea namna mamlaka
hiyo inavyoratibu ukuaji wa sekta ya nyumba kwa kuweka mipango madhubuti ya
matumizi bora ya ardhi kulingana na mahitaji ya Taifa hilo linalotegemea zaidi
utalii.
Mchoro unaoonyesha ramani ya nchi ya Singapore ulioko Makao
Makuu ya Mamlaka ya Uendelezaji nchi hiyo ukionyesha majengo mbalimbali yaliyoko
katika nchi hiyo yenye uhaba mkubwa wa ardhi.
Ujumbe wa Tanzania ukiangalia ramani yenye matumizi
mbalimbali yaliyotengwa kwenye ardhi ya Taifa la Singapore. Katika nchi hiyo
hakuna uwezekano wa mtu yeyote kuvamia kipande chochote cha ardhi kwa kuwa kila
ardhi imepangiwa matumizi yake na kusimamiwa na sheria madhubuti.
Ujumbe wa Tanzania ukitizama maeneo yaliyoendelezwa yenye
matumizi mbalimbali nchini Singapore kwenye jengo la makumbusho ya kihistoria
ya hatua za ukuaji wa mji huo.
Kamishna wa Ardhi Dk Moses Kusiluka(kushoto)na watendaji wa
NHC na Wizara wakipata maelezo kwa njia ya video ya namna mji wa Singapore
ulivyopangwa kulingana na ardhi iliyopo na mahitaji ya Taifa hilo.
Ujumbe wa Tanzania ukiangalia kwa chini mchoro wenye ramani
ya nchi ya Singapore na jinsi matumizi ya ardhi yanavyoratibiwa ulipotembelea
Mamlaka ya Uendelezaji nchi ya Singapore jana.
Makamu wa Rais wa Shirika linalosimamia mipango Miji la
Singapore Bw. Anandan Karunakaran(aliyeinama) akimueleza Waziri Lukuvi maeneo
mapya yaliyotengwa kwa ajili ya uendelezaji mpya wa mji wa Singapore baada ya
kufukia vipande vya bahari(land reclamation) ili kukidhi mahitaji ya sasa na ya
baadaye ya idadi ya watu wa nchi hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni