Jimbo la Utah nchini Marekani
litarejea utekelezaji hukumu ya kifo kwa kupigwa risasi, wakati
ambapo dawa za sindano za kusababisha kifo zitakapokuwa hazipatikani.
Tayari gavana wa Utah ameshatia
saini uamuzi huo kuwa sheria rasmi hapo jana na kuifanya Utah kuwa
jimbo pekee la Marekani linalotekeleza adhabu ya kuuwawa kwa kupigwa
risasi.
Baadhi ya majimbo ya Marekani
yanafikiria kutumia njia nyingine, wakati yakihaha kupata dawa ya
sindano ya kuua, kutokana na kuwepo kwa uhaba mkubwa wa dawa hiyo
Marekani.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni