Mahakama nchini Senegal imemuhukumu
mtoto wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Abdoulaye Wade kifungo cha miaka
sita jela baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na rushwa.
Mtoto huyo Karim Wade pia amepigwa
faini ya dola milioni 230, kwa kujitajirisha visivyo halali wakati wa
utawala wa miaka 12 wa baba yake.
Karim Wade mwishoni mwa wiki
alichaguliwa kuwa mgombea wa urais kwa chama cha upinzani cha PDS.
Rais wa Senegal Macky Sall wiki
iliyopita alionya kuwa serikali yake haitovumilia jaribio lolote la
kuhatarisha usalama wa nchi, baada ya mahakam kutoa hukumu yake.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni